Kuingiza na kuanza kutumia

Kipengele hiki kimekubalika na kurahisishwa pamoja na ruhusa kutoka OpenDroneMap: Maelekezo yaliokosekana, by Piero Toffanin.

Quickstart

Installers for OpenDroneMap are available for purchase from UAV4Geo, and are the easiest way to get started and come with support.

https://opendronemap.org/webodm/download/#installer

That said, OpenDroneMap is a free and open source ecoystem. Community support is available for those looking to install themselves and directions follow:

Sifa za Hardware

Nafasi ndogo inayotakiwa kwa kutumia software ni:

 • 64bit CPU iliotengenezwa sasa au baada ya 2010

 • 20 GB ya kiendshi disk

 • 4 GB RAM

Si zaidi ya picha 100-200 zinaweza kuchakatwa kwa sifa hizo hapo juu (software itafanya kazi kinyume na nafasi). Mahitaji yafuatayo yanapendekezwa:

 • Toleo la sasa la CPU

 • 100 GB za kiendeshi disk

 • 16 GB RAM

Sifa hizo zitaruhusu kwa picha kidogo mia moja kuchakatwa bila uzito mwingi. CPU iliyo na core nyingi itaruhu kuchakata haraka, wakati kadi ya picha (CPU) kwa wakati huo haina faida juu ya utendaji kazi. Kwa kuchakata picha zaidi, engeza kiendshi diski na RAM kulingana na picha unazotaka kuchakata.

Minimum RAM needed for N images

Number of images

RAM or RAM + Swap

40

4

250

16

500

32

1500

64

2500

128

3500

192

5000

256

Uingizaji

Tunapendekeza watu kutumia docker kwa kurun ODM, kama unatumia Windows, macOS au Linux.

Windows

Kutumia OpenDroneMap unahitaji angalau Windows 7. Toleo la nyuma la windows halihimili.

Jia ya 1. Angalia msaada wa uvumbuzi

Docker inahitaji vipengele kutoka kwenye CPU yako inayoitwa virtualization, ambayo inaruhusu kufanya kazi virtual mashine (VMs). Hakikisha unaweka enabled! baadhi ya muda huwa disabled. Kuangalia, katika windows 8 au ya juu zaidi unaweza kufungua Task Manager (Bonyeza CTRL+SHIFT+ESC) na washa Performance tab.

Image of checking virtualization in Windows 8 or higher

Virtualization lazima iruhusiwe

Katika Window 7 kuangalia kama una virtualization ilioruhusiwa, unaweza kutumia Microsoft® Hardware-Assisted Virtualization Detection Tool badala yake.

Ikiwa virtualization haijaruhusiwa, unahitajika uiruhusu. Kwa sasa watoaji ni tofauti kidogo kwa kila aina ya computer, Njia nzuri kufanya hivi ni kuangalia katika search engine “how to enable vtx for <type your computer model here>”. Kawaida muda hutegemea na kurestart computer, haraka bonyeza F2 au F12 wakati inawaka,angalia boot menu na badilisha mpangilo kwa kuruhusu virtualization (kawaida inaitwa "VT-X").

Table of different bios keys

Key iliyozoeleka kubonyeza kwa kuwasha computer kutumia boot menu kwa watengezaji wengi wa PC

Njia ya 2. Ingiza Vinavyohitajika

Kwanza, Unahitaji kuingiza:

Kwa Python 3, hakikisha unaangalia Add Python 3.x to PATH wakati wa uingizaji.

Screenshot of Python3 installation process

Usisahau kuingiza Python executable katika PATH (kwa maana hio unaweza kurun camand pamoja).

Kisha, ikiwa upo katika Windows 10 home pekee, Windows 8 (toleo lolote) au Windows 7 (toleo lolote), ingiza:

Ikiwa upo katika Windows 10 Professional au toleo jipya, unaweza kuingiza badala yake:

Tafadhali usingize programu zote za docker. Ni tofauti na utatengeneza tatizo ikiwa zote zimeingizwa.

Baada ya kuingiza docker, fungua kutoka Desktop icon ambayo imetengenezwa ilipoingizwa (Docker Quickstart kwa Docker Toolbox, Docker for Windows kwa docker kwa ajili ya Windows). Hii ni muhimu, usikatishe hatua hii. ikiwa kuna makosa fuata haraka katika koo na uyatatue.

Njia ya 3. Angalia nafasi na mgao wa CPU

Docker katika Windows inafanya kazi kwa kufungua VM katika msingi (Fikiria VM kama “computer emulator”). VM hii ina kiwango fulani cha nafasi kilichogaiwa na WebODM, kinaweza kutumika tu kwa kiasi ambacho kimetengwa.

Ikiwa utaingiza Docker Toolbox (angalia chini ikiwa utaingiza Docker badala ya windows):

 1. Fungua VirtualBox Manager application

 2. Right click default VM na bonyeza Close (ACPI Shutdown) kusimamisha mashine

 3. Right click default VM na bonyeza Settings...

 4. Move the Base Memory slider from the System panel and allocate 60-70% of all available memory, optionally adding 50% of the available processors from the Processor tab also

Screenshot of VirtualBox Settings

Chaguo msingi la VirtualBox kwa Mpangilio wa VM

Kisha bonyeza OK", right click default VM na bonyeza Start.

Ikiwa umeingiza Docker kwa Windows badala yake:

 1. Angalia mpangilo uteo na bonyeza kulia “white whale” icon.

 2. Kutoka menu, bonyeza Settings...

 3. kutoka kwenye ubao, bonyeza Advanced na tumia sliders kuonesha 60-70% ya nafasi inayotumika na tumia nusu ya CPU ilobakia.

 4. Bonyeza Apply.

Screenshot of Docker Icon

Njia ya 1. Docker icon

Screenshot of Docker Settings

Njia ya 3 & 4 Mpangilo wa Docker

Njia ya 4. Pakua WebODM

Fungua Git Gui programu iliyoingizwa pamoja na Git. Kutoka hapo:

 • Ikifunguka Git Gui, bonyeza 'Clone Existing Repository' option

 • Nani ya Source Location andika: https://github.com/OpenDroneMap/WebODM

 • Ndani ya Target Directory bonyeza browse na tembea hadi folder ulilochagua (tengeneza moja kama lazima)

 • Bonyeza Clone

Screenshot of Git Gui

Git Gui

Ikiwa kupakua kumefanikiwa, utaona window ifuatayo:

Screenshot of Git Gui after successful download

Git Gui baada ya kufanikiwa kupakua (clone)

Nenda hadi Repository menu, kisha bonyeza Create Desktop Icon. Hii itakuruhusu kurudi nyuma kwenda katika application hii kiurahisi zaidi baadae.

Njia ya 4. Zindua WebODM

Kutoka Git Gui, nenda kwenye Repository menu, kisha bonyeza Git Bash. Kutoka kwenye mstari wa camand aina ya terminal:

$ ./webodm.sh start &

Vipengele tofauti vitapakuliwa katika mashine yako katika hatua hii, ikiwemo WebODM, NodeODM na ODM. Baada ya kupakua utapeleka kwa screen zifuatazo:

Screenshot of after successfully downloading WebODM

Console output baada ya kuanzisha WebODM kwa mara ya mwanzo

 • Ikiwa unatumia docker kwa Windows, fungua browser kwenda http://localhost:8000

 • Ikiwa unatumia docker Toolbox, tafuta anuani IP kuunganisha kwa kuandika:

$ docker-machine ip

Utapata jawabu kama ifuatavyo:

192.168.1.100

Kisha utaunganisha kwa http://192.168.1.100:8000 (badilisha anuani IP kuweka iliyo sahihi zaidi).

macOS

Modem nyingi (post 2010) za Mac computer zinafanya kazi MacOS Sierra 10.12 au kubwa inafanyakazi OpenDroneMap kutumia docker, ikiwa hardware virtualization inakubali (angalia chini).

Jia ya 1. Angalia msaada wa uvumbuzi

Fungua terminal window na andika:

$ sysctl kern.hv_support

Utapata jawabu inayofanana na ifuatavyo:

kern.hv_support: 1

Ikiwa jawabu ni kern.hv_support: 1, Mac yako inakuali! Endelea na step ya 2.

Ikiwa majibu ni kern.hv_support: 0, inamaanisha Mac yako ni ya zamani sana kwa kutumia OpenDroneMap. :(

Njia ya 2. Ingiza Vinavyohitajika

Kuna programu mbili tu za kuingiza:

 1. Docker: https://download.docker.com/mac/stable/Docker.dmg

 2. Git: https://sourceforge.net/projects/git-osx-installer/files/

Baada ya kuingiza docker itaona icon ambyo muonekano wake kama nyumbani katika task bar.

Screenshot of Docker whale

Docker app running

Unaweza kuhakikisha kwamba docker inafanya kazi sawa kwa kufungua Terminal app na kuanza kuandika:

$ docker run hello-world

Ambayo itarejesha

Hello from Docker!

Kuhakikisha git imeingizwa, njia fupi:

$ git --version

Ambayo itarejesha kitu sawa kwa ifuatavyo:

git version 2.20.1 (Apple Git-117)

Ikiwa umepata “bash: git: command not found”, jaribu kuwasha tena Terminal app yako na angalia kwa mara nyengine ikiwa kuna makosa wakati wa mchakato wa kuingiza.

Njia ya 3. Angalia nafasi na mgao wa CPU

Docker katika macOS inafanya kazi kwa kuwasha VM katika background (fikiria hilo kama computer emulator”). VM hii ina kiwango cha nafasi kilichowekwa na WebODM inaweza kutumia nafasi ya kutosha iliotengwa.

 1. Right click ikoni ya nyumbani kutoka kwenye task bar na bonyeza Preferences...

 2. Chagua Advanced tab

 3. Rekebisha CPU slider kwa kutumia nusu ya CPU inayopatikana na nafasi ya kutumia 60-70% ya nafasi yote ilyobakia

 4. Bonyeza Apply & Restart

Screenshot of Docker advanced settings

Docker advanced settings

Njia ya 4. Pakua na fungua WebODM

Kutoka Terminal andika:

$ git clone https://github.com/OpenDroneMap/WebODM
$ cd WebODM
$ ./webodm.sh start

Kisha fungua web browser kwenda http://localhost:8000.

Linux

OpenDroneMap inaweza kufanya kazi kwenye Linux yoyote ambayo inaruhusu docker. Kwa mujibu wa nyaraka za website ya docker kwa mujibu wa msaada rasmi uliothibitishwa ni CentOS, Debian, Ubuntu na fedora, pamoja na bainari tuli zinazotumika kwa wengine. Ikiwa unataka kuchakua distribution peke yake kwa kumia OpenDroneMap, Ubuntu ni chaguo la kutumia.

Hatua 1. Mahitaji ya kuingiza

Kuna program nne ambazo zinahitaji kuingizwa:

 1. Docker

 2. Git

 3. Python (2 or 3)

 4. Pip

Hatuweza kuweza kumaliza mchakato wa uwingizaji kwa kila usambazaji wa Linux nje ya hapo, kwa hio tutazuiya maelekezo kwa wote kusambaza wanasaidiwa na docker. Katika kesi zote ni jambo la kufungua terminal prompt na kuandika comand.

Ingiza ndani ya Ubuntu / Debian

Camand za kuandika

$ sudo apt update
$ curl -fsSL https://get.docker.com -o get-docker.sh
$ sh get-docker.sh
$ sudo apt install -y git python python-pip
Ingiza ndani ya CentOS / RHEL

Camand za kuandika

$ curl -fsSL https://get.docker.com -o get-docker.sh
$ sh get-docker.sh
$ sudo yum -y install git python python-pip
Ingiza ndani ya Fedora

Camand za kuandika

$ curl -fsSL https://get.docker.com -o get-docker.sh
$ sh get-docker.sh
$ sudo dnf install git python python-pip
Ingiza ndani ya Arch

Camand za kuandika

$ sudo pacman -Sy docker git python python-pip

Njia ya 2. Angalia Mahitaji ya Ziada

Kwa kuongezea kwa programu tatu juu, dockercompose script pia inahitajika. Baadhi ya muda inakuwa ishahifadhiwa ndani ya docker, lakini kuna muda haijaingizwa. Kuthibitisha kama imeingizwa jaribu kuandika:

$ docker compose --version

Unaweza kuona kitu kinachofanana kama ifuatavyo:

docker compose version 24.0.5, build ced0996600

Njia ya 3. Pakua na zindua WebODM

Kutoka aina ya terminal:

$ git clone https://github.com/OpenDroneMap/WebODM
$ cd WebODM
$ ./webodm.sh start

Kisha fungua web browser kwenda http://localhost:8000.

Camand za msingi na utatuzi shida

Kitu kizuri kuhusu kutumia docker ni 99% ya kazi unayohitaji kufanya ikiwa unatumia WebODM, inaweza kufanywa kwa kutumia ./webodm.sh script. Unaweza kutimiza moja kati ya hizo:

$ ./webodm.sh start

Kuwa makini kuanzisha WebODM na kupanga mpangilio wa msingi wa kuchakata node (node-odm-1). Ikiwa unahitaji kusimamisha WebODM, unaweza kukisia comand gani ya kutumika:

$ ./webodm.sh stop

Kuna camand tofauti unaweza kutumia, kutumia flag tofauti. Flag ni parameter ilipitia kwa ./webodm.sh command na kawaida prefixed with “–”. port flag kwa mfano kufundisha kutumia WebODM katika port za mitandao tofauti:

$ ./webodm.sh start --port 80

Camand nyengine muhimu zimeorodheshwa chini:

# Restart WebODM (useful if things get stuck)
$ ./webodm.sh restart

# Reset the admin user's password if you forget it
$ ./webodm.sh resetadminpassword newpass

# Update everything to the latest version
$ ./webodm.sh update

# Store processing results in the specified folder instead of the default location (inside docker)
$ ./webodm.sh restart --media-dir /path/to/webodm_results

# See all options
$ ./webodm.sh --help

Jukwaa la kijamii ni sehemu nzuri kuomba msaada ikiwa umekwama wakati unapingiza kwa mpangilio na kwa maswali ya ujumla kutumia ./webodm.sh script.

Habari, WebODM!

Baada kuwa inatumika ./webodm.sh ikianza na kufungua WebODM ndani ya browser, utasalimia pamoja na ujumbe wa karibu na utaulizwa kutengeneza mtumiaji wa kwanza. Chukua muda kumalizia mwenyewe pamoja na web interface na kuchunguza menu tofauti.

Screenshot of WebODM Dashboard

WebODM Dashboard

Tazama kwa Processing Nodes menu kuna "node-odm-1" node tayari zishapangwa kwa ajili yako kutumia. NodeODM node hii na imetengenezwa wenyewe kwa WebODM. Node hii inatumika katika mashine moja kama WebODM.

Ikiwa umefikia hapo, Hongera! Sasa ni mda wa kuanza kuchakata baadhi ya data.

Image of celebratory dance

Kuendesha mashine zaidi ya moja

Optionally: Ikiwa una computer nyengine, unaweza kurejea mchakato wa uwingizaji (install docker, git, python, etc.) na anzisha NodeODM mpya kwa kuandika kutoka dirisha la Terminal/Git Bash:

docker run --rm -it -p 3000:3000 opendronemap/nodeodm -q 1 --token secret

Camand hio hapo juu inaiambia docker kuanzisha container mpya kutumia opendronemap/nodeodm picha kutoka docker Hub (toleo la sasa la NodeODM), kutumia port 3000, Panga namba ya juu ya kazi nyingi kwa wakati mmoja hadi 1 na kulinda node kutoka kwenye matumizi yaliozuiwa kutumia password "secret".

Kutoka WebODM kisha unawesha kuwasha Add New button juu ya Processin Nodes Kwa hostname/IP aina ya anuani ya field katika computer nyengine. Kwa port field type "3000". Kwa token field type "secret". Pia unaweza kuengeza label kwa node yako, kama vile computer ya pili. Kisha bonyeza Save.

Ikiwa kila kitu kimeenda sawa, lazima uwe na processing node mbili! Utaweza kuchakata kazi nyingi kwa wakati mmoja kwa kutumia mashine tofauti.

Learn to edit and help improve this page!